Wednesday, 27 September 2017

MAPINDUZI YA TRAP KATIKA MUZIKI RAP...........>>>>

Muziki wa kufoka foka al maarufu kama muziki wa rap ulibuniwa nchini Marekani ambapo ilikuwa katika lengo la kujitetetea na shughuli za utumwa.Watu waliobuni stail hiyo ya kuimba ambayo hapo mwanzo walikuwa wakizungumza kwa staili hiyo ambapo maneno ya mwisho yalikuwa yakikatwa kwa maana inamuwia vigumu mtu ambaye sio muhusika kusikia kwa mfano neon mama lilitamkwa ma.
Kwanini leo tunauzungumzia muziki huu?Hii ni kwasababu ya mapinduzi yanaendelea kufanywa na wasanii na watunzi wa aina hii ya muziki.Kwa takribani miaka mingi sana staili ya uimbaji imekuwa ikibadilika sana.Hii imesababisha hata wale waasisi wa muziki huu kuwa na wasiwasi huenda muziki huu ukaja ukapotea kabisa katika ramani ya dunia.

Mwanzoni wa miaka ya 2010 ndipo yalipoanza mapinduzi makubwa ya aina mpya ya muziki wa rap ambapo uliingiliwa na staili mpya ya uimbaji ikijulikana kama TRAP RAP staili ambayo hata motto anaweza kuimba lakini kitakachomshinda ni kuitendea haki beat(mdundo)Wengi tuliipenda sana staili hii mpya hasusani baada ya kumsikia msanii kama T.I alipoileta aina hii muziki kwa namna yake.
Mapinduzi ya TRAP yalikuwa ni makubwa lakini kitu kinachoifanya TRAP kuchukiwa na waasisi wa muziki wa RAP kama Snoop Doggy ni kukosekana na ujumbe ndani ya muziki.Ikumbukwe kuwa RAP ilibuniwa ili kufikisha ujumbe flani na kwa kipindi kirefu RAP imekuwa ikitetea watu weusi nchini Marekani lakini pia ilikuwa ikiburudisha ambapo kwa kizazi cha kina 50 Cents,YG,Lil Wayne na wengineo ndo kizazi kilichoifanya RAP kuwa muziki wa biashara ambapo waliburudisha zaidi lakini pia walifikisha ujumbe kwa jamii na jamii ilijifunza juu ya maswala kadhaa kama unyanyasaji wa kijinsia,ufisadi nk
Hali imekuwa tofauti katika TRAP ambapo ni aina ya muziki unao burudisha kwa asilimia 99.9 na asilimia 0.1 ikawa ndo kufikisha ujumbe kwa wasikilizaji na wapenzi wa muziki huo ambapo umezalisha wasanii wengi sana kama FUTURE,DESIGNER,MIGOS,T.I n.k Hali hii imewafanya waasisi wa muziki wa RAP kuikataa aina hii ya muziki kwamba haijatoka katika zao lao kwani inakiuka misingi ya RAP.

Mjadala ulikuwa mkubwa hasa pale linapokuja kuuweka muziki wa TRAP katika kundi lipi.Maana wasanii wa muziki huu wamekuwa wakifoka lakini wanaimba kawaida pia.Waasisi wa RAP wakikataa kuunga mkono muziki huo lakini wasanii na watunzi nao wakiendeleza juhudi zao katika kuendeleza muziki huo na kuufanya kuwa muziki unaopendwa zaidi duniani.
Dunia nzima sasa inauimba na kuucheza muziki wa TRAP kuliko hata aina nyingine ile ya muziki.Hii ina maana kwamba muziki wa TRAP umetawala duniani na unasikilizwa zaidi.Mapinduzi haya yameweza kufanikiwa kama yalivyofanikiwa kwa muziki wa RAP.
Mpaka sasa sijasikia muasisi wa RAP kafanya TRAP na endapo itatokea itamaanisha kuwa wamekubalina na aina hii ya muziki ambao umewakamata vijana wengi wa kizazi cha kijitali.Kwa mtazamo wangu waasisi hawa waendeleze muziki wa TRAP kwani kuna maswala mengi yanatokea duniani na yanahitaji kukemewa kwa aina ya mashairi na wao ndo wana nafasi kubwa kutunga na kuimba kwa ajili ya ukombozi wa dunia na muziki wa RAP.Binafsi nna uheshimu muziki wa RAP kwani umekuza vizazi vingi sana  mpaka wasanii wa TRAP ni zao la RAP licha ya waasisi wa RAP kukikataa kizazi hiki.
Swali linalonijia ni kwamba JE MUZIKI HUU UTADUMU KAMA ILIVYODUMU RAP?Majibu ya swali hili nawaachia wadau wa muziki ambao ndio wana nafasi kubwa kukuza muziki na kudidimiza muziki katika kila sekta sio TRAP tu.

0 comments: