Sunday, 19 November 2017

IFAHAMU ZAIDI..."Koenigsegg Agera R" Gari inayokwenda kasi zaidi duniani

IFAHAMU ZAIDI
"Koenigsegg Agera R" Gari inayokwenda kasi zaidi duniani

Wiki iliyopita tulilitazama gari aina ya Tata Namo ambayo ni gari ya bei nafuu zaidi duniani leo acha tuangalie gari inayokwenda kasi zaidi duniani ambapo kwa sasa kasi kubwa ni kilomita 270 kwa lisaa.
Kampuni ya koenigsegg kutoka nchini Sweden ambayo iligunduliwa mwaka 1994 na mmiliki na mbunifu wake anajulikana kwa jina Christian Von Koenigsegg.Kampuni hii ina makao makuu ndani ya mji wa Angelholm.Kampuni hii ndiyo inayoongoza kwa kutoa magari yenye kasi zaidi duniani ambayo ni ya kimichezo(sport cars) zaidi moja aina ya magari hayo ni kama Koenigsegg CC,Koenigsegg CC8S,Koenigsegg Agera RS na Koenigsegg Agera R.

Leo nataka tuliangalie gari aina ya Koenigsegg Agera R ambayo limeundwa na kampuni ya Koenigsegg ambayo ndo iliweza kuandikwa kwenye kitabu cha Guinness mwaka 2005 baada ya kuizidi gari aina ya McLaren F1 ambayo lina kasi ya kilomita 386.4 kwa lisaa ambalo liliundwa mwaka 1998.
Koenigsegg Agera R ni gari ambayo iliundwa mwaka 2011 ambayo iliundwa kwa muundo wa kimashindano lakini ni gari flani ya kifahari zaidi pia.Gari hii imekuja na injini ya 5-Lita yenye uwezo wa Turbo.Gari hili lina uwezo wa kwenda mbio sawa na farasi 1200 ambayo ni sawa na na mita 186 chini ya sekunde 11 ambayo ni rekodi ya dunia mpka sasa.
Christian Von Koenigsegg mmiliki wa kampuni ya Koenigsegg 
Gari hili lina uwezo wa kwenda kasi kwa kilomita 300 mpaka kilomita 433 kwa saa na pia lina injini yenye uwezo wa kufanya magurudumu yote kuzungunguka kwa wakati mmoja kitu ambacho ni nadra sana katika magari mengi hata yale ambayo yanayokwenda kasi kama Buggati na Ferrari.Gari hili lina milango miwili ambayo inafunguka kwa juu mfano wa mabawa,gari hili lina wastani wa uzito wa kilo 1,395 na lina urefu wa mita 4.293 upana wa mita 1.996 na kimo cha mita 1.12.
Kuweza kumiliki gari hili unahitaji kuwa na bajeti ya takribani kiasi cha dola za kimarekani milioni 1.7 sawa na shilingi bilion 3.8 za kitanzania.Gharama ya gari hili imekuwa ikiwatesa watu wengi hasusani wale wanaopenda mashindano na michezo ya magari,Kwa mujibu wa mtandao maalumu wa Koenigsegg gharama hii imehusishwa na ubora wa gari lenyewe pamoja na usala wake,kwa taarifa yako tu ni kwamba Christian Von Koenigsegg hajawahi kutamani kuendesha gari tofauti na magari ya kampuni yake mwenyewe
Koenigsegg Agera R
Koenigsegg Agera R muonekano wa ndani





0 comments: